" Hizi hapa Takwimu za Mchezaji Mpya wa Yanga Allan Okello, ni balaa

Hizi hapa Takwimu za Mchezaji Mpya wa Yanga Allan Okello, ni balaa

 

TAKWIMU ZA ALLAN 𝗢𝗞𝗘𝗟𝗟O ZINATISHA ✍️

Nyota wa timu ya Taifa ya Uganda, Allan Okello yupo kwenye form bora zaidi ya maisha yake ya soka. Amehusika moja kwa moja katika mabao 10 kwenye mechi zake 10 za mwisho akiwa na Uganda “The Cranes”. Wakati katika michezo yake 20 ya awali alikuwa na G/A 4 .

Mechi zake 10 za mwisho akiwa na timu ya taifa ya Uganda .

◉ 10 – Michezo
◉ 10 – Goli + asisti
◉ 06 – Goli
◉ 04 – Asisti

— Alikuwa mfungaji bora katika ligi kuu ya Uganda msimu uliopita wa 24|25 baada ya kufunga mabao 19 — ni mara ya kwanza katika career yake kufikisha double figures ya mabao (mabao 10+) katika kampeni moja ya ligi .

— Na pia akawa mchezaji wa kwanza wa Vipers kufunga zaidi ya magoli 18 kwenye msimu mmoja wa ligi katika kampeni 10 zilizopita .

📊 ➜Takwimu zake ngazi ya klabu na timu ya taifa tangu ulipoanza msimu uliopita .

*Michezo : 34 mabao 19, asisti 3 (Goli+pasi – 22) – Vipers SC

*Michezo : 11 – Mabao 06 , asisti 4 (Goli + pasi 10) – Uganda the Cranes

Jumla : Michezo 45, Mabao 25, Asisti 7 (Goli+Pasi 32)

  • Ukiangalia Takwimu za Allan Okello zinakupa tafsiri kuwa ni Mchezaji wa daraja la juu sana , ambaye anaweza kuanza katika vikosi vyote vya timu za Vilabu Afrika mashariki. Unaweza kuwa na hoja zako binafsi kuhusu ubora wa ligi anayotokea lakini usisahau kuwa kipaji cha mpira hakichagua mahali pakuwaka.

Post a Comment

Previous Post Next Post