
Taarifa kutoka Tunisia zinasema kuwa kocha wa Young Africans, Pedro Goncalves ni miongoni mwa makocha waliotuma maombi rasmi kwa shirikisho la mpira wa miguu Tunisia (FTF) kwa ajili kuomba nafasi ya kuifundisha timu ya taifa ya Tunisia.
Ikumbukwe timu ya taifa ya Tunisia kwa hivi sasa haina kocha mkuu, na hii imefuatia baada ya kuachana na aliyekuwa kocha wao Sami Trabelsi.
Licha ya Pedro Goncalves kutuma maombi hayo lakini majina makuu ambayo yanajadiliwa kwa ukaribu zaidi na FTF ni majina ya makocha watatu wa Kifaransa ambao ni Sabri Lamouch, Willy Sagnol pamoja na Frank Haise.
Sabri Lamouch ndiye kocha ambaye anaonesha kuwa anauhitaji zaidi wa kuifundisha timu hiyo ambayo imeshafuzu World Cup, hii ni baada ya kuwaambia viongozi wa FTF kuwa yupo tiyari kupunguziwa gharama za mshahara wake ili aifundiahe timu hiyo.
Kocha mwengine ambaye jina lake lipo kwenye meza ya FTF likijadiriwa ni Neserdine Nabi, yeye ni miongoni mwa makocha ambao wanatazamiwa kuchukuwa nafasi ya Sami Trabelsi ya kukinoa kikosi hicho kuelekea kwenye mashindano ya kombe la dunia.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment