Na,Egidia Vedasto,
Misalaba Media,Arusha.
Katika muendelezo wa usafi Jijini Arusha Meya wa Jiji hilo Maxmillian Iranqhe amewapongeza wananchi wa Kata ya Daraja mbili pamoja na viongozi wao kwa mazingira yao kuonekana kuwa safi tofauti na kata zingine.
Amesema hayo katika kituo cha afya Daraja mbili ambapo usafi umefanyika mahali hapo na kuwataka wananchi suala la kusafisha mazingira kuwa endelevu.
"Naendelea kuwakumbusha Afisa watendaji wote wa kata hii wasimamieni wananchi khaki Misha wanafanya usafi katika maeneo yao kabla ya kufungua na kufunga biashara ili kuhakikisha Jiji linakuwa safi kila wakati,"
"Katika utendaji wenu pia jiepusheni na rushwa, kila mmoja awajibike kwa haki" amesema Iranqhe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Alinyanya Masoud Sungwa a melon text wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usafi wa Kituo Kituo cha Afya cha Daraja mbili, pamoja na juhudi za halmashauri ya Jiji kuhakikisha usafi unaimarishwa.
Sambamba na hayo ameomba vifaa vya hospitalini ikiwemo genereta kubwa ili kuendesha shghuli za kituo pindi umeme unapokatika, kuunganishwa kwa mtandao wa maji taka kati ya shule ya sekondari na kituo cha afya pamoja na X-Ray.
"Kipekee nawashukuru sana kutukumbuka Kata ya Daraja mbili na kutuunga mkono katika suala la usafi, tunaomba miti ya kutosha tuweze kuotesha katika Kata yetu ili kuendana na lengo la Arusha kuwa ya kijani" amesema Sungwa.
Katika namna hiyohiyo Daktari wa kituo cha Afya Daraja mbili Luciana Kazimoto ameshukuru muitikio mkubwa wa wananchi katika kusafisha mazingira ya kituo hicho na kuhakikisha yanakuwa safi.
"Natamani suala hili lisiwe na ukomo bali liwe endelevu, pia naomba mtukumbuke miundombinu yetu sio mizuri, Kwa maana ya vifaa vya hospitali na "paving" kwa mazingira ya kituo" amesema Dr.Kazimoto.
Vilevile Barozi wa shina namba 11mtaa wa Alinyanya Nerina Shafii amesema ataendelea kusisitiza usafi kufanyika kila wakati kila mmoja katika eneo lake.
"Naomba serikali iangalie kwa jicho la pekee miundombinu ya kata yetu, ikiwemo vivuko na daraja maana wagonjwa na wanafunzi ndio waathirika wakubwa, Nina na serikali hii naamini kila kitu kitatekelezwa kwa wakati" amesema Merina.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment