" JIMOTOLI AHAMASISHA VIJANA KUIMARISHA UMOJA NA MSHIKAMANO NDANI YA CCM

JIMOTOLI AHAMASISHA VIJANA KUIMARISHA UMOJA NA MSHIKAMANO NDANI YA CCM

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Ndugu Jimotoli Jilala Maduka, tarehe 21 Januari 2026 alimwakilisha Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi kama Mgeni Rasmi katika Kikao cha Kawaida cha Baraza la Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Mpanda, kikao cha kufunga mwaka 2025.

Akizungumza katika kikao hicho, Ndugu Jimotoli Jilala Maduka aliwasisitiza vijana wa CCM Wilaya ya Mpanda kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa pamoja katika utekelezaji wa majukumu ya Jumuiya na Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla, akieleza kuwa nguvu ya chama inajengwa kupitia mshikamano, nidhamu na ushirikiano wa wanachama wake, hususan vijana.

Ndugu Jimotoli alihimiza vijana wa UVCCM kuwa mstari wa mbele katika kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi, zikiwemo fursa za ajira, ujasiriamali, mikopo ya vikundi vya vijana na miradi ya maendeleo inayotolewa na Serikali, akisema vijana wana nafasi kubwa ya kujenga mustakabali wao kupitia juhudi, maarifa na ubunifu.

Aidha, Ndugu Jimotoli Jilala Maduka alimpongeza Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uongozi wake thabiti, wenye maono na unaozingatia maendeleo ya vijana, amani na ustawi wa Taifa.

Pia amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia imeendelea kuweka mazingira rafiki kwa vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kijamii, jambo linalopaswa kuungwa mkono kwa vitendo.

Amewasihi vijana wa CCM Wilaya ya Mpanda kuendelea kulinda heshima ya chama, kuwa mabalozi wazuri wa sera na mwelekeo wa CCM katika jamii, pamoja na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na maendeleo ya wananchi huku akisisitiza umuhimu wa nidhamu, maadili mema na uzalendo kama msingi wa uongozi bora ndani ya chama.

Baadhi ya viongozi wa UVCCM Wilaya ya Mpanda walimshukuru Mgeni Rasmi kwa ushauri na hamasa aliyotoa, wakiahidi kuendeleza umoja na mshikamano, kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo na kuimarisha mchango wa vijana katika kukijenga na kukitetea Chama Cha Mapinduzi.

Kikao hicho cha kufunga mwaka 2025 kinatumika pia kufanya tathmini ya shughuli za UVCCM kwa mwaka mzima, kuweka mikakati ya mwaka 2026 na kuimarisha ushirikiano kati ya jumuiya za CCM Wilaya ya Mpanda kwa ajili ya maendeleo ya chama na wananchi kwa ujumla.




 

 

Post a Comment

Previous Post Next Post