" KAMPENI YA MAMA SAMIA LEGAL AID YAWANOA WANASHERIA TAMISEMI, HALMASHAURI KUFUATA

KAMPENI YA MAMA SAMIA LEGAL AID YAWANOA WANASHERIA TAMISEMI, HALMASHAURI KUFUATA

Na Egdia Vedasto, 

Misalaba Media, Arusha 

Katibu Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI Adolf Ndunguru amewataka Mawakili waliopewa mafunzo kuhusu namna bora ya kuendesha kampeni ya Samia Legal Aid kuviishi viapo vyao Kwa mujibu wa Sheria na miongozo iliyopo.


Ndunguru ameyasema hayo Jana Jijini hapa wakati akifunga mafunzo ya siku tatu Kwa Mawakili na wanasheria kutoka Tamisemi na sekretarieti za Mikoa waliohudhuria mafunzo hayo ikiwa ni maandalizi ya kampeni hiyo iliyoanza tangu mwaka 2023.

Aidha Katibu Mkuu Ndunguru amewataka kuepuka vishawishi vya rushwa vinavyoweza kupoteza Haki za wananchi, “ lengo kuu ni kuwarudishia wananchi tabasamu,” amesema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Eliakim Maswi amesema Wizara yake imejiandaa kutokomeza kabisa migogoro ya ardhi nchini kupitia kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid.

Maswi amesema migogoro ya ardhi imekuwa tatizo kubwa nchini na imekuwa ikisababisha ugomvi katika jamii na kuondoa amani iliyokuwepo.

“ Katika awamu ya kwanza na ya pili ya zoezi la kampeni ya kutoa msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid, migogoro ya ardhi ilionekana kuwa kinara dhidi ya malalamiko mengi yaliyokuwa yakihitaji msaada wa kisheria,”

Amesema tofauti na awamu zingine za kampeni hiyo, awamu hii migogoro itakayowasilishwa wataalam wa Sheria watahakikisha wanaifuatilia kuanzia mwanzo hadi mwisho wake Ili isiweze kujirudia kabisa.

Maswi amesema katika mafunzo ya siku tatu Jijini Arusha waliyopewa Mawakili na wanasheria hao wa Serikali ni pamoja na kuhakikisha wanaondokana na rushwa kupitia kampeni hiyo Ili kuweza kutenda Haki Kwa wote.

Amesema Ili kuifanya kampeni hiyo kuwa endelevu na kuipa ngivu zaidi, wizara ya Katiba iliamua kushirikisha mamlaka za Mikoa pamoja na Tamisemi.

Maswi amesema hadi kufikia Juni mwaka Jana 2025, zaidi ya wananchi Milioni 4 waliwasilisha maombi yao katika kampeni hiyo wakihitaji msaada wa kisheria na kwamba miongoni mwa migogoro iliyowasilishwa migogoro ya ardhi ilikuwa ikiongoza.

“ Migogoro iliyofuatia baada ya ardhi ni mirathi na pia changamoto ya ndoa, na ndio sababu tukaamua kuwaita wenzetu wa sekretarieti za Mikoa kwa kushirikiana na Tamisemi na baadae tutaita Halmashauri zote Kwa kuwa Hawa wote ndio wako karibu na wananchi,” amesema.

Amesema kampeni hiyo awali haikuwa ikitatua migogoro hadi mwisho kwa kuwa ilikuwa ikifanyika katika ngazi ya kitaifa lakini hivi sasa migogoro yote itamalizwa Hadi mwisho kwa kuwa itakuwa ikifanyika Kwa ngazi ya Mkoa na Serikali za mitaa

“”Ikumbukwe kuwa Rais wetu ana nia njema na wananchi wake, ndio maana aliamua kuipa kampeni hii jina lake (Mama Samia Legal Aid) na kufikia mwezi wa sita mwaka Jana wananchi Milioni 4.1 walipata msaada, na tunatarajia kupitia kwenu wananchi wengi waweze kunufaika”amesema.


Post a Comment

Previous Post Next Post