
Kocha wa Timu ya Singida Black stars Miguel Gamondi ameendelea kuweka historia ya kipekee katika nchi ya Tanzania, zifuatazo ni rekodi za Gamondi hapa Tanzania.
Ya kwanza, amefanikiwa kuiongoza Yanga kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika msimu wa 2023/24 baada ya kumfunga Al- Merrikh ya Sudan na kuifanya Yanga kutinga hatua ya makundi.
Ya pili, Kaiongoza Yanga kutinga hatua ya robo Fainali kwa mara ya kwanza mbele ya kundi gumu ambalo lilikuwa na vigogo kama Al ahly, Cr Belouizdad pamoja na medeama ya Nchini Ghana na Yanga ilitinga robo Fainali kwa jumla ya Pointi nane.
Ya tatu, Gamondi akaondoka Tanzania halafu akarejea Tena baada ya kurejea ikawa zamu ya Singida Black stars kufaidi Mbinu zake akaipa Singida Black stars kombe la CECAFA kagame Cup 2025 baada ya kuwafunga Al hilal Omdurman katika uwanja wa KMC Complex.
Ya Nne, Gamondi akapewa dhamana ya kuongoza majeshi kuelekea nchini Morocco kwaajili ya AFCON 2025 akiwa kama kocha mkuu stars ilikusanya jumla ya pointi 2 katika kundi C lakini ikafanikiwa kutinga katika hatua ya 16 bora kwa mara ya kwanza. Katika hatua hiyo amepangwa dhidi ya Morocco January 4 je atafanya maajabu yake?
HHuyu ndiyo master @miguelgamondi mzee wa mtoto Kautaka.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment