Mkurugenzi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa, amesisitiza kuwa vyama vya siasa ni washindani na si maadui. Ameshauri vyama vyote—tawala na upinzani—kufuata misingi ya sheria katika kudai haki.
"Kudai haki zako hakukupi ruhusa ya kuharibu mali au kudhuru watu wengine; haki lazima iambatane na wajibu," alisisitiza Olengurumwa.
Serikali tayari imeahidi kuunda tume ya maridhiano ili kurejesha umoja wa kitaifa, hatua inayoungwa mkono na wadau wa siasa kama njia ya pekee ya kuijenga upya Tanzania.
Pamoja na kauli hiyo wapo wadau wanaobainisha wazi kuwa ushiriki wa vijana katika vurugu unadhoofisha uchumi wao na wa taifa ukizingatia kwmaba wao ndio kundi kubwa na lenye uwezo mkubwa wa kuleta maendeleo.Takwimu za Sensa ya 2022 zinaonesha kuwa 34.5% ya Watanzania ni vijana (miaka 15-35) na wanajumuisha 55% ya nguvu kazi ya taifa.
Mchambuzi wa masuala ya kijamii, Thomas Kibwana, anafafanua kuwa uharibifu wa miundombinu hulazimisha serikali kutumia fedha za walipakodi kufanya matengenezo badala ya kufadhili miradi mipya ya maendeleo.
Naye Rahma Mshamu, mwanafunzi wa SJMC, anatoa wito kwa kila mwananchi kukataa uchochezi na kutanguliza maslahi ya taifa. Aidha, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kenani Kihongosi, amewataka vijana kuwa makini na taarifa wanazopokea na kusambaza ili kulinda utulivu wa nchi.
Baadhi ya wananchi na wadau wa maendeleo nchini wametoa wito wa kudumisha amani na kurejea kwenye meza ya maridhiano, wakibainisha kuwa vurugu hazina mshindi na huleta majuto makubwa kwa taifa na uchumi wa mtu mmoja mmoja.
Hayo yanakuja kufuatia kundelea kujitokeza kwa masimulizi ya kusikitisha kutoka kwa mashuhuda wa vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025, wakati wa Uchaguzi Mkuu, ambapo mali ziliharibiwa na taharuki kutawala katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo mkoani Songwe.
Funzo la Vurugu: Amani haina Mbadala
Joel Daudi, mkazi wa Ileje, anasimulia kuwa vurugu zina uwezo wa kufuta juhudi za miaka mingi ndani ya sekunde chache. "Niliona hofu machoni mwa watu... madhara ya vurugu ni makubwa kuliko sababu yoyote inayotolewa kuhalalisha vurugu," anasema Joel.
Naye Juliana Jimmy wa Tunduma anaeleza kuwa bila juhudi za vyombo vya dola, hali ingekuwa mbaya zaidi kwani biashara zilifungwa na watu walikimbia kutafuta usalama. Masimulizi haya yanatoa fundisho kuwa haki haipatikani kwa fujo, bali kwa njia ya mazungumzo na maridhiano.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment