Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Diwani wa Kata ya Kivule, Rajabu Manyinya, ameweka mkazo katika uwezeshaji wa vijana kiuchumi na kijamii kwa kuimarisha sekta ya usafiri, afya na elimu, akisema maendeleo ya kata hiyo hayawezi kupatikana bila kundi hilo kushirikishwa kikamilifu.Manyinya ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Bodaboda na Bajaji cha Bomba Mbili (Mwanzo Mgumu),Kivule uliofanyika Januari 24, 2026, ambapo amesema katika awamu ya uongozi wake amejipanga kuhakikisha anatumia vyema fursa na Imani aliyopewa na wananchi ili kuwaletea maendeleo.Diwani huyo amewapongeza vijana wa kituo hicho kwa kuzingatia nidhamu na kuamua kuunda kituo rasmi, akieleza kuwa hatua hiyo imeongeza usalama, uwajibikaji na heshima kwa waendesha bodaboda na bajaji katika eneo hilo.Amesema baada ya kukamilika kwa zoezi la usajili, vijana wanaostahili watapatiwa bodaboda ili kuwawezesha kufanya kazi kwa tija na kujiondoa katika vitendo visivyo halali.Katika kuimarisha huduma za kijamii, Manyinya ametangaza kufunguliwa kwa dirisha la usajili wa bima ya afya, akisema vijana wamepewa kipaumbele ili kuhakikisha wanapata matibabu kwa gharama nafuu. Ameeleza kuwa mwanachama mmoja atachangia shilingi 40,000 kwa mwaka, huku kifurushi cha watu sita kikiwa ni shilingi 150,000.Aidha, amesema serikali imeandaa mpango maalum kwa makundi maalum yatakayopata huduma za afya bila malipo, ikiwemo huduma ya kuchukua miili ya marehemu bure.Kuhusu masuala ya utambulisho, diwani huyo amesema zoezi la kuandikisha na kugawa vitambulisho vya NIDA limepangwa kuanza Januari 2, 2026 katika Ofisi za Kata ya Kivule (Misitu), likilenga wananchi wenye namba za NIDA ambao bado hawajapata vitambulisho.Katika sekta ya elimu na afya, Manyinya amesisitiza kuwa mpango wa ujenzi wa zahanati pamoja na shule ya msingi na shule ya sekondari katika eneo la Bomba Mbili bado upo, na ameahidi kuhakikisha miundombinu hiyo inatekelezwa kwa ubora unaostahili.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bomba Mbili, Hassan Shamte, amesema kituo cha bodaboda na bajaji kimeundwa na vijana wenye nidhamu na maadili mema, akieleza kuwa ni mfano wa vijana waliodhamiria maendeleo.Naye Mwenyekiti wa Kituo cha Bodaboda cha Bomba Mbili, Julius Mbwira, amesema kuwa kituo hicho kimejikita katika kupambana na matumizi ya dawa za kulevya, lugha chafu na vitendo vya uhalifu, huku akibainisha kuwa kwa sasa wana wanachama 23 waliosajiliwa.Ameongeza kuwa bado kuna vijana watiifu lakini hawana bodaboda, hivyo wameomba kuungwa mkono ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment