Wananchi wa Kata ya Mchoteka wilayani Tunduru wameishukuru Serikali kupitia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuboresha huduma za msingi za kijamii ambazo awali zilionekana kuwa ndoto kwa muda mrefu katika kata hiyo.
Shukrani hizo zimebainishwa wakati Wilaya ya Tunduru ikiadhimisha ya miaka 49 ya Chama Cha Mapinduzi, ambapo kilele cha maadhimisho hayo kinatarajiwa kufanyika tarehe 5 Februari mwaka huu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi wa Kata ya Mchoteka wameeleza kuridhishwa kwao na uboreshaji wa huduma za afya katika kituo cha afya cha kata hiyo, hali ya mawasiliano kuwa ya uhakika pamoja na kuimarika kwa sekta ya elimu kufuatia ujenzi wa shule za msingi na sekondari.
Wananchi wamesema ujenzi wa shule hizo umepunguza adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu, jambo ambalo limeongeza hamasa ya wazazi kuwapeleka watoto wao shule na kuboresha kiwango cha ufaulu kwa ujumla.
Hata hivyo, pamoja na mafanikio hayo, wananchi wamebainisha kuwepo kwa changamoto kadhaa ikiwemo huduma ya maji safi na salama, ambapo mradi wa maji upo lakini bado haujasambazwa katika vijiji vyote vya kata hiyo, pia miundombinu ya barabara, ambapo baadhi ya barabara hazipitiki kipindi chote cha mwaka, hali inayokwamisha shughuli za kiuchumi na maendeleo ya wananchi, na hivyo kuiomba Serikali na chama kusimamia kwa karibu utatuzi wa changamoto hizo.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mchoteka, Mhe. Seif Dauda, amewataka wananchi kuungana kwa pamoja katika kuleta maendeleo,
'kwa yule anaodhani kuwa maendeleo ya kata ya Mchoteka yanaletwa na mtu mmoja huyo hatatuchelewesha, hakuna maendeleo ya watu wengi yanayoweza kuletwa na mtu mmoja "
Aidha amewataka wenyeviti wa vijiji kuwa wabunifu katika maeneo yao ili kuweza kuhakikisha maendeleo yanawafikia kwa wakati akieleza kuwa kufanya hivo kutaongeza utendaji wa kazi
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment