Bank of Africa Tanzania imeshiriki katika maadhimisho ya wiki ya Huduma ya Kifedha yaliyoandaliwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango yaliyofanyika katika viwanja vya Usagara vilivyopo jijini Tanga.Yakiwa na kauli mbiu isemayo “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi,” malengo makuu ya maadhimisho hayo yalikuwa ni kuongeza uelewa, kuboresha ufahamu na hatimaye kuhamasisha mabadiliko ya tabia za wananchi katika usimamizi wa fedha na matumizi ya huduma rasmi za kifedha.Aidha, tukio hilo lililenga kuwahamasisha Watanzania kutumia huduma rasmi za kifedha kama sehemu ya jitihada za kupunguza kiwango cha umaskini katika jamii, ili kufikia maendeleo ya kiuchumi jumuishi na endelevu.Mwisho

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment