Mafundi wa kutengeneza Magari Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu ya kuwa Mabalozi wa usalama barabarani Kwa kutoa taarifa za vyombo vya moto vilivyosababisha ajali na kwenda kutengenezwa kificho.Elimu hiyo imetolewa na Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila ambapo amewataka kuacha tabia ya kupokea Magari mabovu ya wateja ambayo yanaonekana kuwa yamefanya ajali sehemu na kwenda kurekebishwa pasipo kuwa na taarifa kutoka Polisi.Sajenti Ndimila amewaeleza kuwa kuyapokea Magari hayo na kuyatengeneza yalipo haribika pasipo kuwa na taarifa sahihi kama yamefanya uhalifu wa barabarani inasababisha kutokujulikana Kwa mhalifu kwani Magari hayo yanaweza kuwa yamegonga vyombo vingine vya moto, wanyama, watembea Kwa miguu pia hata miundombinu barabarani kama milingoti ya taa za barabarani na Kingo za madaraja.Aidha Mafundi hao wamejurishwa kuwa ushirikiano wao unahitajika sana kwani kufanya hivyo kutasaidia kubainika Kwa waharifu wa makosa ya barabarani lakini pia kusaidia kupunguza ajali za barabarani.Kwa upande wao Mafundi wa Magari wamepongeza Kwa hatua ya Jeshi la Polisi ya kuwafikishia elimu hiyo na kuahidi kutoa ushirikiano kuwabaini wakosaji hao pia itawaweka salama katika maeneo yao ya kazi.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment