Na Lydia Lugakila, Misalaba MediaMBEYAMahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya imefanya bonanza kubwa la michezo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria mwaka 2026.Bonanza hilo limefanyika Januari 31, 2026 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) kilichopo mkoani Mbeya, na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya sheria pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo.Akizungumza katika bonanza hilo, Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya, Bi. Aziza Temu, amesema lengo kuu la bonanza hilo ni kuimarisha umoja na mshikamano kati ya Mahakama na wadau wengine wa sheria, wakiwemo mawakili wa Serikali na mawakili wa kujitegemea, kupitia michezo pamoja na kubadilishana mawazo.Bi. Temu ameongeza kuwa mashindano hayo ni endelevu na yameandaliwa na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya, huku akihimiza jamii kujenga utamaduni wa kushiriki michezo ili kujijenga kiafya, kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja pamoja na Taifa kwa ujumla.Kwa mujibu wa Bi. Temu, michezo iliyoshindaniwa kupitia bonanza hilo ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa pete, karata, bao, drafti, kuvuta kamba, michezo ya watoto pamoja na michezo mingine mbalimbali.Ameeleza kuwa baadhi ya michezo hiyo ilishirikisha timu kutoka Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, Mahakama ya Mkoa wa Songwe, Chama cha Wanasheria wa serikali (PBA)pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society – TLS) mkoani humo, ambapo michezo kama mpira wa miguu, mpira wa pete, na kuvuta kamba ilipata ushindani mkubwa.Bi. Temu amesema bonanza hilo pia lililenga kukuza uchumi kwa kuwapa fursa wajasiriamali kuuza bidhaa na huduma mbalimbali katika eneo la tukio, ikiwa ni mchango wa Mahakama katika ustawi wa maendeleo ya Taifa.Kauli mbiu ya bonanza hilo ilikuwa ni “Mchango wa Mahakama katika Ustawi wa Maendeleo ya Taifa.” ambayo ndio kauli mbiu ya siku ya sheria kwa mwaka 2026Hata hivyo, washindi wa mashindano hayo, ikiwemo mpira wa miguu na mpira wa pete, walipatiwa vikombe huku washindi wa mchezo mingine wakipatiwa medali.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment