Imeandaliwa na: Mervat SakrJamhuri ya Kiarabu ya Misri inaanza rasmi kushika urais wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kuanzia tarehe Februari 1, 2026 kwa kipindi cha mwezi mmoja. Urais wa Misri unakuja katika wakati nyeti unaoshuhudia kuongezeka kwa changamoto za kiusalama, kisiasa na kimaendeleo barani Afrika, sambamba na mazingira ya kikanda na kimataifa yaliyochangamana, yanayohitaji ushirikiano wa karibu na mshikamano wa juhudi za pamoja ili kukabiliana na changamoto hizo. Inatarajiwa kuwa kipindi cha urais wa Misri kitashuhudia mjadala wa masuala mengi muhimu katika nyanja za kisiasa, kiusalama, kimaendeleo na kimazingira.Urais wa Misri unalenga kuimarisha ufanisi wa Baraza la Amani na Usalama kama chombo kikuu chenye dhamana ya kudumisha utulivu na kuimarisha amani barani Afrika, kupitia mkabala jumuishi unaolenga kuendeleza muundo wa amani, usalama na utawala bora barani Afrika, kwa namna itakayochangia katika usuluhishi wa migogoro, kuimarisha usalama na utulivu, pamoja na kufanikisha malengo ya Ajenda ya Umoja wa Afrika ya Maendeleo 2063.Aidha, urais wa Misri wa Baraza la Amani na Usalama utazingatia kuakisi misingi na kanuni thabiti zilizomo katika Hati ya Msingi ya Umoja wa Afrika, zinazojengwa juu ya kuheshimu mamlaka ya nchi wanachama, umoja wao na ulinzi wa ardhi zao, kulinda taasisi zao za kitaifa, kutoingilia masuala ya ndani, na kuimarisha utekelezaji wa kazi za pamoja katika mfumo wa Umoja wa Afrika, jambo litakalosaidia katika kudumisha amani, usalama na kufikia maendeleo endelevu.Inatarajiwa pia kwamba urais wa Misri utaandaa mfululizo wa shughuli na vikao vya kina vitakavyoshughulikia maendeleo ya hali nchini Sudan na Somalia. Katika muktadha huu, mashauriano yasiyo rasmi yatafanyika katika ngazi ya mawaziri wa Baraza hilo pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, yakifuatiwa na vikao viwili vya mawaziri vitakavyolenga kujadili maendeleo ya hali nchini Sudan na Somalia. Hii ni pamoja na kupitishwa kwa ripoti ya mwaka ya shughuli za Baraza la Amani na Usalama, itakayowasilishwa na ujumbe wa Misri katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (Mkutano wa Afrika).Aidha, mpango wa urais wa Misri unajumuisha kuandaa vikao vya Baraza kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabianchi, amani na usalama; mafaili ya ujenzi upya na maendeleo baada ya migogoro ambayo Misri inayaongoza; pamoja na masuala ya akili mnemba (Artificial Intelligence), utawala bora, amani na usalama. Vilevile, mashauriano yatafanyika na idadi ya mashirika maalumu kujadili uhusiano kati ya usalama wa chakula, amani na usalama, pamoja na kukabiliana na changamoto za mpito wa kisiasa katika nchi za Afrika, sambamba na utekelezaji wa shughuli, mashauriano na ziara za uwanjani ambazo urais wa Misri utaendelea kuratibu kwa ushirikiano na wadau husika.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment