" MBUNGE WA JIMBO LA BUKENE, MHE. JOHN STEPHANO LUHENDE, KWA KUSHIRIKIANA NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA WARUDISHA TABASAMU KWA WAHANGA WA KIMBUNGA KATA YA KASELA

MBUNGE WA JIMBO LA BUKENE, MHE. JOHN STEPHANO LUHENDE, KWA KUSHIRIKIANA NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA WARUDISHA TABASAMU KWA WAHANGA WA KIMBUNGA KATA YA KASELA

                                          Na. Elias Gamaya – Nzega, Tabora

Mbunge wa Jimbo la Bukene, Mhe. John Stephano Luhende, kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, Rtd SSP Aron Maganga, imetembelea na kuwafariji wahanga wa kimbunga kilichosababisha uharibifu mkubwa wa makazi katika Kata ya Kasela, Kijiji cha Nindo, Kitongoji cha Kaselya.

 Ziara hiyo imefanyika kufuatia tukio la upepo mkali uliotokea usiku wa Januari 05, 2026, ambapo nyumba kadhaa za wananchi ziliezuliwa paa na nyingine kubomoka kabisa, na kuwaacha wananchi wengi katika hali ngumu ya maisha.

 Katika ziara hiyo, Ofisi ya Mbunge imetoa pole kwa wahanga na kuwahakikishia ushirikiano wa hali na mali, hususan katika juhudi za kukarabati na kurejesha makazi yaliyoharibiwa na janga hilo. Hatua hiyo imelenga kupunguza athari za tukio hilo na kurejesha matumaini kwa wananchi waliokumbwa na maafa.

Aidha, Ofisi ya Mbunge imetoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti, kuepuka ukataji ovyo wa miti na uchomaji wa misitu, hatua ambazo ni muhimu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi yanayochangia majanga kama kimbunga na ukame.

Katika hatua nyingine Mhe. Luhende amewahakikishia wananchi ushirikiano usiokoma, upendo wa dhati na dhamira ya kweli ya kuwaletea maendeleo kwa vitendo, huku akisisitiza kuwa ofisi yake itaendelea kuwa karibu na wananchi katika nyakati za furaha na changamoto.












 

Post a Comment

Previous Post Next Post