Fabius Clavery,Misalaba Media-Kagera.
Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba imetaja miradi ya kimkakati yenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 inayotekelezwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi, kuongeza fursa za ajira na kukuza mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji katika mkutano wa Baraza la Madiwani kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa Fedha 2025/2026,Oktoba–Disemba, uliofanyika Januari 29, 2026 katika ukumbi wa Chemba, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Bi. Fatina Hussein Laay, amesema miradi hiyo ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha uchumi wa wananchi na kukuza maendeleo ya maeneo yanayochipukia kimaendeleo.
Bi. Fatina amesema miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa ghala la dagaa pamoja na ununuzi wa mashine ya kukaushia dagaa katika eneo la Igabilo, ujenzi wa soko la ndizi Kemondo, uendelezaji wa stendi ya Kemondo pamoja na ujenzi wa jengo la kitega uchumi Shablidin.
Ameeleza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unalenga kuongeza thamani ya mazao na bidhaa za wananchi hususan dagaa na ndizi, kuimarisha biashara ndogo na za kati pamoja na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri.
Aidha, Bi. Fatina amesema kupitia miradi hiyo, Halmashauri inatarajia kuongeza ajira kwa vijana na wanawake sambamba na kuchochea ukuaji wa miji katika maeneo ya vijiji vinavyoendelea kukua kiuchumi.
Mkutano huo wa Baraza la Madiwani uliwakutanisha madiwani, wakuu wa idara na vitengo pamoja na wataalamu wa Halmashauri, ambapo ulipokea na kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment