Na, Egidia Vedasto,
Misalaba Media, Arusha
Waziri wa maliasili na utalii Dkt.Ashatu Kijaji ameitaka mamlaka ya uhifadhi ya Ngorongoro kuendelea kuimarisha ulinzi wa ikolojia ya mimea na wanyama hatua itakayoongeza watalii na kufikia milioni nane ifikapo mwaka 2030.
Amesema hayo katika tukio la kuvishwa cheo, uapisho wa Kamishna wa uhifadhi na uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi Ngorongoro (NCAA) lililofanyika Arusha.
Aidha amewataka watumishi hao kutenda kazi kwa ushirikiano na kujali utu. Kuhakikisha wawekezaji wanaongezeka, utalii unakua na uchumi kukua kiwango cha kutosha.
"Nawaamini katika utendaji wenu, Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anategemea kuona mapinduzi nakubwa katika mamlaka hii, si hivyo tu, Bali kila Mtanzania ana imani na Bodi hii" amesema Dkt.Kijaji.
Hata hivyo amepongeza hatua ya mapato kukua kutoka bilioni 250-350 na kwamba matarajio ni kuona mapato yanakua zaidi.
Kwa upande wake Kamishna wa mamlaka ya uhifadhi ya Ngorongoro Abdul Razak Badru amesema atahakikisha wanatekeleza maagizo yote ili kufikia malengo ya watalii na mapato kuongezeka.
Amesema kuwa wataenzi na kudumisha uhai na historia ya Mamlaka ya uhifadhi Ngorongoro kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
"Naahidi kuwa tutatua matatizo, tutaimarisha ushirikiano na kuongeza thamani ya mamlaka hiyo. Kipekee nanmshukuru Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Mstaafu Generali Venance Mabeyo kwa mara nyingine kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa mamlaka ya uhifadhi ya Ngorongoro, ni imani yangu kuwa tutayafikia malengo" amesema Kamishna Badru.
Katika namna hiyo hiyo Mwenyekiti mteule wa Bodi ya Uhifadhi Ngorongoro Mstaafu Generali Venance Mabeyo ameshukuru kupata Bodi ya Wakurugenzi iliyosheheni wabobezi na wataalam katika sekta mbalimbali tofauti na ilivyo kuwa hapo awali.
Amebainisha kuwa kupitia Bodi hiyo mahiri, ni dhahiri kuwa mageuzi yatakuwa makubwa na chanya. Malengo yanayotarajiwa yatafikiwa kupitia umoja huo.
"Ninaahidi kwamba,tutafanya kazi usiku na mchana kama tulivyoelekezwa na Wakurugenzi hawa watapata mafunzo maalum ya kuwaweka tayari kufanya kazi hii, hakika timu imeshiba na iko tayari kuleta mabadiliko katika Mamlaka ya uhifadhi Ngorongoro" amesema Generali Mabeyo.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment