Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mheshimiwa Joel Nanauka, ameanza ziara ya kikazi mkoani Kagera ambapo ametembelea Wilaya ya Muleba kwa lengo la kukagua na kujionea utekelezaji wa miradi ya vijana inayofadhiliwa kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri.
wakati wa ziara yake wilayani Muleba tarehe 24 Januari 2026,Mhe. Nanauka ameipongeza halmashauri hiyo , akisema imejidhihirisha kuwa mfano bora katika utoaji wa mikopo kwa vijana pamoja na usimamizi madhubuti wa miradi inayotekelezwa.
Akitoa mifano ya miradi hiyo, Waziri Nanauka ametaja mradi wa vijana wa kahawa wa Makongora uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 445, kiwanda cha ufyatuaji wa matofali cha Vijana Magata/Karutanga kilichogharimu shilingi milioni 232, mradi wa usafirishaji wa abiria wa Umoja wa Madereva Muleba (shilingi milioni 85), Umoja wa Madereva wa Taxi Muleba (shilingi milioni 134), pamoja na mradi wa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba uliopo Katembe, Kata ya Kimwani, uliogharimu shilingi milioni 151. Amesema miradi hiyo imeonesha matokeo chanya na kuleta tija kwa vijana wanaonufaika.
Kutokana na mafanikio hayo, Mhe. Nanauka amesema Wizara ya Maendeleo ya Vijana itaendelea kuhimiza halmashauri nyingine nchini kujifunza kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kuhusu utoaji na usimamizi bora wa mikopo ya asilimia 10, ili kuongeza fursa za kiuchumi kwa vijana nchini.
Katika ziara hiyo, Waziri Nanauka ameambatana na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini, Mheshimiwa Adonis Alfred Bitegeko, ambaye amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa kipaumbele kwa sekta ya kilimo. Ameeleza kuwa kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, zaidi ya ekari 300 zimetengwa kwa ajili ya kilimo cha zao la kahawa.
Mhe. Bitegeko pia amepongeza uamuzi wa kuanzishwa kwa Wizara ya Maendeleo ya Vijana, akisema hatua hiyo italeta msukumo mkubwa kwa vijana kujikita katika shughuli za kiuchumi. Ameeleza kuwa mradi wa kahawa wa Makongora ni mfano halisi wa namna vijana wameanza kuamini na kutegemea miradi ya maendeleo kama njia ya kujenga uchumi wao na kupanua fursa za kipato.
Ameahidi kuendelea kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Vijana pamoja na Waziri Joel Nanauka ili kuhakikisha vijana wa Muleba na Tanzania kwa ujumla wanaendelea kuwezeshwa na kufikia malengo yao kupitia fursa mbalimbali za kiuchumi.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment