Muleba Kagera.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mheshimiwa Joel Arthur Nanauka, tarehe 24 Januari 2026, amefanya ziara ya kikazi mkoani Kagera na ametembelea mradi wa ufyatuaji wa tofali unaomilikiwa na vijana wa kikundi cha Umoja wa Vijana Business kilichopo Wilaya ya Muleba.
Katika ziara hiyo, Mhe. Nanauka ametembelea eneo la mradi na amejionea shughuli za uzalishaji wa tofali, huku amepata maelezo ya kina kutoka kwa vijana hao kuhusu utekelezaji wa mradi, changamoto wanazokumbana nazo pamoja na mikakati waliyojiwekea ya kuukuza na kuupanua zaidi.
Akizungumza na vijana hao, Waziri Nanauka amewapongeza kwa ubunifu, bidii na juhudi zao katika kujiajiri kupitia miradi ya uzalishaji, akisisitiza kuwa mradi huo ni mfano bora wa namna vijana wanavyoweza kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo binafsi sambamba na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa.
Aidha, Mhe. Nanauka amezihimiza taasisi za serikali kuendelea kutoa ushirikiano kwa vijana katika utekelezaji wa miradi yao ya kiuchumi. Vilevile, ametoa wito kwa vijana nchini kote kutumia kikamilifu fursa ya mikopo yenye riba nafuu inayotolewa na serikali kupitia Halmashauri zao, kwa lengo la kuanzisha na kukuza miradi ya maendeleo.
Kwa upande wao, vijana wa kikundi cha Umoja wa Vijana Business wameishukuru serikali kwa kuweka mazingira wezeshi yanayowawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji. Wameahidi kuongeza juhudi katika kuendeleza mradi wao, kukuza ajira kwa vijana wenzao na kuongeza pato kwa jamii inayowazunguka.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
.webp)

Post a Comment