
Wenyeji wa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, Morocco, wamefanikiwa kuiondoa Nigeria kwa mikwaju ya penalti 4-2 katika mchezo wa nusu fainali na kufuzu fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.
Hatua hiyo imekuja baada ya timu hizo kucheza dakika 120 bila mshindi kupatikana, hali iliyomlazimu mwamuzi kuamua mshindi kupitia mikwaju ya penalti.
Katika mchezo huo uliochezwa Januari 14, 2026 nchini Morocco, Youssef En-Nesyri alipiga penalti ya ushindi kwa ustadi mkubwa, akiupachika mpira kwenye kona ya chini kushoto. Hii ilikuja baada ya kipa Yassine Bounou kuokoa penalti za Samuel Chukwueze na Bruno Onyemaechi wa Nigeria.
Kwa ujumla, mchezo huo ulikuwa na nafasi chache za wazi, na mapema ilidhihirika kuwa mikwaju ya penalti ingeweza kuamua mshindi.
Mfungaji bora wa michuano hiyo, Brahim Diaz, alikosa nafasi bora ya Morocco kabla ya dakika 30 baada ya kukosea hesabu ya mpira wa kichwa kutoka kwa krosi ya Achraf Hakimi iliyotokea upande wa kulia, huku jaribio lake likigonga zaidi bega badala ya kichwa.
Washambuliaji nyota wa Nigeria, Victor Osimhen na Ademola Lookman, walikuwa na wakati mgumu kupata nafasi, wakipata mipira michache katika mchezo huo.
Kutokana na matokeo hayo, Morocco wataikabili Senegal katika mchezo wa fainali utakaochezwa Jumapili, Januari 18, 2026, baada ya Senegal kuifunga Misri bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment