" MSIFANYE MICHEZO WAKATI WA KUVUKA BARABARANI

MSIFANYE MICHEZO WAKATI WA KUVUKA BARABARANI


Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nhelegani Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu ya kujikinga dhidi ya ajali za barabarani Kwa kuacha kufanya michezo pindi wanapovuka barabara.

Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewasisitiza kukanyana wao Kwa wao pindi wanapoona Kuna mmoja kati Yao akiwa anafanya michezo wakati wa kuvuka barabara.

Aidha Sajenti Ndimila amewaelimisha sehemu sahihi ya kuvukia ambayo ni kwenye alama ya kivuko Cha watembea Kwa miguu na sio kila mtu kuamua kuvuka sehemu anayojisikia yeye ni sahihi kwake.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post