Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma kimeanza rasmi mchakato wa kumpata mgombea ubunge kwa ajili ya uchaguzi mdogo, ambapo uchukuaji na urejeshaji wa fomu umeanza leo tarehe 18 Januari. Mchakato huo umeanza kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Jenista Mhagama, kilichotokea tarehe 11 Desemba 2025.Akizungumza Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Vijijini, Juma Nambairo, amewahimiza wanachama wenye sifa na nia ya kuwania nafasi hiyo kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu na kushiriki katika mchakato huo kwa kuzingatia kanuni na taratibu za chama.Aidha, Nambairo ameendelea kueleza kuwa taratibu za uchaguzi huu ni za kipekee, ambapo uchukuaji wa fomu utafanyika kwa muda wa siku mbili, kabla ya kuanza kwa ratiba ya kura za maoni katika ngazi mbalimbali za chama.

Post a Comment