Madereva wa Magari ya mizigo Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu kuhusu umuhimu wa kutowapatia waajiri wao leseni zao za udereva kama dhamana ya kazi zao.Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewaeleza Madereva hao kuwa leseni hizo za udereva ni hati za kisheria zinazowatambulisha wao uhalali wao wa kuendesha Magari hayo barabarani hivyo ni lazima watembee nazo ili waweze kurahisisha utambuzi wao wanapokaguliwa na Askari barabarani.Aidha Sajenti Ndimila amewataka Madereva hao kuwafikishia elimu hiyo waajiri wao kuwa hawana mamlaka kisheria kuzishikiria leseni hizo za udereva kama dhamana ya kazi zao badala yake kutafuta utaratibu mwingine utakaorahisisha michakato Yao ya dhamana katika kazi hizo.Nao madereva waliopata elimu hiyo wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwafikia na kuwaelimisha vizuri na kuahidi kutekeleza jambo Hilo na na kuondoa usumbufu pindi wanaposimamishwa na Askari barabarani Kwa ajili ya ukaguzi.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment