" MUSEVENI ANAONGOZA MATOKEO YA AWALI ZAIDI YA ASILIMIA 60

MUSEVENI ANAONGOZA MATOKEO YA AWALI ZAIDI YA ASILIMIA 60

Na: Belnardo Costantine, Misalaba Media- Uganda.

Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa Uganda 2026 yanaonyesha Rais Yoweri Museveni wa chama cha NRM anaongoza kwa zaidi ya asilimia 60 ya kura zilizohesabiwa. Matokeo hayo yalitangazwa  kabla ya saa tano usiku.l Kwa sasa za Africa mashariki.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Uganda, Jaji Simon Byabakama, amesema matokeo hayo yanatokana na vituo 133 vya kupigia kura, vinavyowakilisha asilimia 0.26 ya jumla ya kura zote. Aliongeza kuwa taarifa zaidi zitatolewa Ijumaa saa tatu asubuhi, huku matokeo yakiendelea kuwasilishwa katika kituo kikuu cha kuhesabu kura cha Wakiso.

Awali, Tume ya Uchaguzi ilisema zoezi la upigaji kura kwa ujumla lilikwenda vizuri licha ya changamoto za kiufundi, ikiwemo mashine za kupigia kura kushindwa kufanya kazi na kulazimisha matumizi ya njia ya kawaida. Hata hivyo, mgombea wa upinzani Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, amedai uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu, madai ambayo bado hayajathibitishwa na mamlaka husika.

Aidha Matokeo rasmi ya uchaguzi yanatarajiwa kutangazwa ndani ya saa 48 baada ya kukamilika kwa zoezi la upigaji kura huku vyombo vya Usalama nchini  vinaendelea kuimarisha usalama katika Baadhi ya maeneo ambayo yanadhaniwa kuwa na uvunjifu wa amani

Post a Comment

Previous Post Next Post