" MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA KAGERA ASHUKURU SERIKALI KWA MIRADI YA MAENDELEO ,KATIKA DUA MAALUM YA KULIOMBEA TAIFA MKUU WA MKOA AMSIFU

MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA KAGERA ASHUKURU SERIKALI KWA MIRADI YA MAENDELEO ,KATIKA DUA MAALUM YA KULIOMBEA TAIFA MKUU WA MKOA AMSIFU

‎Na Fabius Clavery, Misalaba Media-Kagera ‎Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera, Faris Buruhan amempongeza Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani Katika Dua maalumu ya kuliombea Taifa imefanyika katika Kata ya Katoro, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, ikihusisha viongozi wa dini, viongozi wa serikali pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kagera.‎Akizungumza katika dua hiyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera, Faris Buruhan, Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi kubwa anazoendelea kuzifanya katika kuleta na kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Kagera.‎Katika hotuba yake, Faris Buruhan amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Kagera kwa kujitokeza kwa wingi na kutenga muda wao kuliombea Taifa, akibainisha kuwa sala na dua ni msingi muhimu wa kulinda amani na kuimarisha maendeleo endelevu ya nchi.‎Faris amesema kuwa miradi hiyo imechangia kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi, ikiwemo sekta za afya, elimu, miundombinu na maji, hali ambayo imeongeza ustawi wa wananchi wa mkoa huo. Amesisitiza kuwa maendeleo hayo ni matokeo ya uongozi thabiti, uzalendo na maono ya Rais Samia katika kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli.‎Aidha, Mwenyekiti huyo amewapongeza viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali waliojitokeza kushiriki katika dua hiyo, akisema mchango wao ni muhimu katika kudumisha amani, mshikamano na maadili mema katika jamii. Vilevile aliwapongeza viongozi wa serikali kwa ushirikiano wao katika shughuli za kijamii na kiroho kwa manufaa ya Taifa.‎Dua hiyo ilifanyika, tarehe 31 Desemba 2025, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajjat Fatuma Mwassa. Katika hotuba yake, amewahimiza wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa mkoani humo.‎Kadhalika mkuu huyo wa Mkoa amepongeza jitihada na uwezo mkubwa alionao  Faris kuwa ni hazina kubwa kwa Taifa la Tanzania.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post