" Kero za Barabara Kuwa Historia Bukene: OFISI YA MBUNGE JIMBO LA BUKENE YAANZA TATHMINI KUTATUA KERO SUGU ZA BARABARA.

Kero za Barabara Kuwa Historia Bukene: OFISI YA MBUNGE JIMBO LA BUKENE YAANZA TATHMINI KUTATUA KERO SUGU ZA BARABARA.

Na. Elias Gamaya Nzega, Tabora

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Bukene, chini ya uongozi wa Mhe. John Stephano Luhende, kwa kushirikiana na Mhandisi Mwandamizi kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Nzega, Eng. Makunge Mwera, imefanya ziara ya kikazi ya kutembelea, kubaini, kufanya tathmini na kuchukua hatua za awali za kutatua kero sugu za miundombinu ya barabara ndani ya Jimbo la Bukene.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Bukene, Katibu wa Mbunge, Ndugu Abubakary Bukuku, amesema kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa miundombinu ya barabara katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi, hivyo haitaacha kushirikiana na wataalam wa TARURA kuhakikisha changamoto zote zinazokwamisha usafiri na usafirishaji zinatatuliwa kwa wakati.

Ndugu Bukuku ameongeza kuwa Mbunge wa Jimbo la Bukene anaendelea kuchukua hatua madhubuti kwa kushirikiana na TARURA ili kuhakikisha barabara zote zenye changamoto zinafanyiwa kazi kulingana na hali halisi, ikiwemo kuanza matengenezo ya haraka pale inapowezekana na kuandaa mipango ya muda mrefu kwa barabara zinazohitaji uwekezaji mkubwa zaidi.

Katika hatua nyingine, Ndugu Bukuku amesema kuwa kwa barabara ambazo zinasubiri kupokea fungu kutoka Serikalini pamoja na zile ambazo bado hazijapangiwa bajeti maalum, Mhe. John Stephano Luhende ameahidi kupanua wigo wa ushirikiano na wataalam wa TARURA kwa kuomba mfuko maalum wa barabara na fedha za maendeleo, ili kuhakikisha miradi mbalimbali ya miundombinu ya barabara inakamilika na kuleta tija kwa wananchi wa Jimbo la Bukene.

Wananchi wa kata zilizotembelewa wamepongeza juhudi za Mbunge wao kwa kuwafuata hadi katika maeneo yao, kusikiliza kero zao moja kwa moja na kuchukua hatua za vitendo, wakieleza kuwa jitihada hizo zimeongeza imani, matumaini na ari ya kushiriki katika kulinda na kuendeleza miundombinu ya barabara katika jimbo lao.

Ziara hiyo ni sehemu ya mkakati wa Mbunge wa Jimbo la Bukene wa kuhakikisha changamoto za barabara zinatatuliwa kwa uwazi, ushirikishwaji wa wananchi na kwa maslahi mapana ya maendeleo ya Jimbo la Bukene.

 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post