" OFISI YA MBUNGE JIMBO LA BUKENE YASHIRIKI KIKAO MAALUM CHA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE KWA WANAFUNZI WENYE UHITAJI – NZEGA

OFISI YA MBUNGE JIMBO LA BUKENE YASHIRIKI KIKAO MAALUM CHA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE KWA WANAFUNZI WENYE UHITAJI – NZEGA

Na. Elias Gamaya -Nzega, Tabora

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Bukene, chini ya Mheshimiwa John Stephano Luhende imeshiriki kikao maalum kilichoandaliwa na kuratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Mheshimiwa Naitapwaki Tukai, chenye lengo la kupanga na kuratibu mpango wa pamoja wa kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji vifaa vya shule.

 Lengo kuu la kikao hicho ni kushirikiana kati ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Ofisi za Wabunge wa majimbo yote ya Wilaya ya Nzega katika kutatua changamoto ya upungufu wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wanaotoka kwenye mazingira magumu pamoja na wenye mahitaji maalum, hususan kuelekea muhula mpya wa masomo wa Januari, 2026.

 Kikao kazi hicho pia kilihusisha maandalizi ya ziara maalum itakayofanywa shule kwa shule, ikilenga kuwabaini, kuwafikia na kuwasaidia wanafunzi wote wenye uhitaji. Ziara hiyo inatarajiwa kuongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega kwa kushirikiana na Wabunge wa majimbo yote ya wilaya hiyo.

 Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Nzega, Ndugu Winfrida Emmanuel Funto, pamoja na Makatibu wa Wabunge wa majimbo yote ya Nzega, ambao ni Katibu wa Jimbo la Bukene Ndugu Abubakary Ally, Katibu wa Jimbo la Nzega Mjini Ndugu Yohana Lulyeho na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini Ndugu Lenatus Dotto.

 

 

 

Post a Comment

Previous Post Next Post