
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limetoa ufafanuzi wa taarifa inayosamba kwenye mtandao wa kijamii wa TikTok ikidai Msanii wa muziki Shilole kupata ajali ya gari na kujeruhiwa akiwa safarini akitokea Mkoani Kigoma akielekea Mkoani Dodoma ambapo gari aliyokuwa akiitumia kwa safari aina ya Toyota Alphad ambayo namba zake za usajili bado hazijafamika iligonga Ngombe eneo la Maragalasi wilayani Uvinza.
Taarifa hiyo ya Polisi inasema ,”Ukweli ni kwamba taarifa hiyo ya ajali haijaripotiwa kituo chochote cha Polisi Mkoa wa Kigoma, hata hivyo tunashauri dereva yeyote anapopata ajali akiwa safarini ambayo imepelekea kifo, majeruhi au uharibifu wa chombo anawajibu wa kutoa taarifa Kituo cha Polisi ili aweze kupata msaada wa matibabu, kuchunguza chanzo cha ajali na kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa mtuhumiwa aliyesababisha ajali.,”
Polisi wametoa wito kwa Shilole kufika kituo chochote cha Polisi kuripoti ajali hiyo, ili uchunguzi uweze kufanyika na hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa mtuhumiwa aliyesababisha ajali hiyo.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limewataka madereva wa vyombo vya moto mkoani Kigoma kuendelea kutii na kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali ambazo zinaweza kutokea kutokana na uzembe wa madereva
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment