" Rais Samia Awapa Milioni 500 Wachezaji Taifa Stars kwa Kufuzu 16 Bora

Rais Samia Awapa Milioni 500 Wachezaji Taifa Stars kwa Kufuzu 16 Bora

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameizawadia timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) shilingi milioni 500 kufuatia kufanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora katika michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON).

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 03, 2026 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwigulu Nchemba, wakati akizungumza na wachezaji pamoja na benchi la ufundi la Taifa Stars kwa njia ya simu.

Waziri Mkuu Dkt. Nchemba amesema kuwa, Mheshimiwa Rais amewapongeza Wachezaji, Benchi la ufundi pamoja na Watanzania wote kwa mafanikio hayo ya kihistoria na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono timu hiyo.

Aidha, Waziri Mkuu ameongeza kuwa, Rais Dkt. Samia ameahidi kutoa zawadi nono zaidi endapo Taifa Stars itaendelea kufanya vizuri na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Morocco.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post