
Jeshi la Polisi limemwachia kwa dhamana Thadey Kweka, ambaye ni raia wa Marekani mwenye asili ya Tanzania.
Raia huyo alikuwa akishikiliwa tangu Desemba 28, 2025 katika Kituo Kikuu cha Polisi Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo uchochezi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kuachiwa kwake leo Januari 3, 2026.
“Ni kweli tumemwachilia kwa dhamana leo kutokana na tuhuma mbalimbali zilizokuwa zinamkabili,” amesema Kamanda Maigwa.
Taarifa za kukamatwa kwa Kweka zilitolewa Desemba 29, 2025 na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime baada ya kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba mwananchi huyo ambaye anaishi nchini Marakeni alitekwa mkoani humo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda Maigwa imeeleza kuwa Kweka alikamatwa kutokana na tuhuma za jinai zilizokuwa zikimkabili, mojawapo ikiwemo uchochezi.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment