" SENEGAL YATINGA FAINALI YA AFCON 2025 BAADA YA USHINDI

SENEGAL YATINGA FAINALI YA AFCON 2025 BAADA YA USHINDI






Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Senegal imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya Misri katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa, Januari 14, 2026, nchini Morocco.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji nyota Sadio Mané katika dakika ya 78, baada ya kupiga shuti kali nje ya eneo la mita 18 lililomshinda mlinda mlango wa Misri.

Katika mchezo huo, Senegal walitawala mchezo kuanzia kipindi cha kwanza hadi mwisho wa dakika 90.

Kwa ushindi huo, Senegal sasa wanamsubiri mshindi kati ya Nigeria na Morocco ili kukutana naye katika fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Post a Comment

Previous Post Next Post