
Senegal ilianza kwa kufungwa mapema kipindi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Sudan. Hata hivyo, kabla ya mapumziko walifanikiwa kusawazisha na kuongeza bao jingine.
Mchezo wa hatua ya 16 bora kati ya Senegal na Sudan umemalizika kwa Senegal kushinda kwa mabao 3–1. Bao la kuongoza kwa Sudan lilifungwa na Aamir Abdallah.
Senegal walisawazisha dakika ya 29, kisha wakaongeza bao la pili dakika ya 45+3 kupitia Pape Gueye. Bao la tatu la Senegal lilifungwa kipindi cha pili na Ibrahim Mbaye dakika ya 77.
Mchezo huo uliochezwa katika Grand Stade de Tanger ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo Senegal walipata jumla ya kona 7, huku Sudan wakipata kona 4 ndani ya dakika 90.
Kesho, Januari 4, 2026, Timu ya Taifa ya Tanzania itakuwa kazini kusaka tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali, wakivaana na Morocco, ambao ni wenyeji wa mashindano hayo
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment