
Habari za hivi punde zinaeleza kuwa wachezaji wa timu ya taifa ya Algeria, kupitia shirikisho lao la soka, wamemwandalia zawadi ya dola za Kimarekani 20,000 kutokana na ubunifu wake wa kipekee. Tukio hili linaonyesha jinsi ushabiki wake unavyovuka mipaka na kugusa mataifa mengine nje ya DRC.
Kiasi hiki cha fedha kikigeuzwa katika sarafu ya Tanzania ni zaidi ya Shilingi Milioni 40, kiasi ambacho kinatajwa kutosha kabisa kumsaidia mbunifu huyo kujenga nyumba au kugharamia masomo ya watoto wake kwa miaka mingi. Wadau wa michezo mitandaoni wamepongeza hatua hiyo wakisema kuwa “ukiwa mbunifu sio rahisi kufa njaa,” huku wakiona zawadi hiyo kama mtaji mkubwa wa biashara kwa shabiki huyo.
Habari hii imezua gumzo kubwa huku watu wakilinganisha mafanikio ya Kuka Lumumba na mashabiki wengine, wakishauri kuwa ni heri kuwa mbunifu kuliko kubaki na mazoea. Zawadi hii kutoka kwa wachezaji wa Algeria inathibitisha kuwa jitihada na rangi za kuvutia anazoonyesha Kuka Lumumba uwanjani zimepata thamani kubwa ya kimataifa. Huu ni mfano tosha wa jinsi michezo inavyoweza kuunganisha watu wa mataifa tofauti kupitia sanaa na ushabiki.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment