Leo Jumamosi Januari 17, 2026, kikundi cha SHY TALENT
FILMS kimeendelea na mazoezi ya utayari wa kutengeneza filamu na tamthilia,
hatua inayolenga kuendeleza vipaji vya vijana na kuibua vipaji vipya katika
Manispaa ya Shinyanga.
Mazoezi hayo yamefanyika katika ofisi za Misalaba
Media, Mjini Shinyanga, na kuhusisha washiriki wengi kutoka kwenye kikundi,
ikiwa ni pamoja na waigizaji, walimu wa sanaa na viongozi wa kikundi ambapo kila
mshiriki amejikita katika kujifunza mbinu za maigizo, uelewa wa script, na
maadili ya kazi ya sanaa.
Akizungumza wakati wa mazoezi, Mkurugenzi wa Misalaba
Media, Mapuli Misalaba, amesisitiza umuhimu wa nidhamu, mshikamano na ubora wa
kazi katika safari ya kuendeleza vipaji.
Mwenyekiti wa SHY TALENT FILMS, Daniel Elimbopo,
amewashukuru washiriki wote kwa moyo wao wa kujitolea na kujitambua, huku
akisisitiza kuwa mazoezi haya ni hatua ya kwanza kuelekea kutengeneza filamu na
tamthilia zenye ujumbe wa kijamii na elimu.
Pia ameeleza kuwa kikundi hiki ni darasa la maisha kwa
vijana, si burudani pekee, bali jukwaa la kujenga fikra, uelewa na weledi wa
sanaa.
SHY TALENT FILMS ni kikundi cha sanaa kilichoanzishwa
na Misalaba Media, chombo cha habari cha mtandaoni kinachotumia sanaa na
ubunifu kama nyenzo ya kuelimisha, kuhamasisha na kuibua vipaji vya vijana.
Kwa taarifa zaidi kuhusu shughuli za kikundi hiki,
tembelea ukurasa wao wa Instagram: SHY TALENT FILMS.
“Kuibua vipaji leo, Kujenga wasanii wa kesho.”

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

















Post a Comment