" ZAIDI YA VIJANA 200 MBEYA WANUFAIKA NA AJIRA KUPITIA MGODI WA ABT CHUNYA WAMPONGEZA MMILIKI

ZAIDI YA VIJANA 200 MBEYA WANUFAIKA NA AJIRA KUPITIA MGODI WA ABT CHUNYA WAMPONGEZA MMILIKI

Na Lydia Lugakila -Misalaba media MbeyaZaidi ya vijana 200 wameeleza kufanikiwa kuendesha maisha yao baada ya kupata ajira kupitia mgodi wa uzalishaji mawe unaomilikiwa na Kampuni ya ABT (Alliance Brilliant and Transparent), uliopo eneo la Matundasi, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya.Akizungumza wakati wa ziara ya Misalaba Media iliyofika mgodini hapo kujionea shughuli mbalimbali za uchimbaji, Januari 17,2026 Vijana hao wameipongeza kampuni ya ABT kwa mchango wake mkubwa katika kuwawezesha kiuchumi kupitia ajira, sambamba na kuwajali wafanyakazi wake pale wanapokumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo magonjwa.Kwa mujibu wa vijana hao, kampuni imekuwa ikitoa huduma muhimu ikiwemo matibabu, chakula pamoja na msaada mwingine wa kijamii unaowasaidia kuendelea na kazi zao kwa ufanisi.Vijana wapongeza uongozi wa Kampuni ambapomiongoni mwa vijana hao ni Kurwa Sady Seleman, mchimbaji wa uchorongaji mawe, mzaliwa wa Mkoa wa Tabora, ambaye amemshukuru mmiliki wa kampuni hiyo, Ambwene Mwaijulu, kwa kuwapatia vijana wengi fursa ya kujipatia kipato cha halali.Kijana huyo amesema ajira katika mgodi huo haihitaji shahada ya juu bali inahitaji nguvu, akili na juhudi, jambo linalowapa nafasi vijana wengi wasio na elimu ya juu. Aidha, ameeleza kuridhishwa na huduma za afya wanazopatiwa, huku akiomba kupatiwa vifaa vya kujikinga na vumbi kama barakoa (mask) wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.Kwa upande wake, Rajab Rashid, msimamizi wa mgodi kutoka Mkoa wa Tabora, amesema kupitia ajira zinazotolewa na ABT, baadhi ya vijana wameweza kuwapatia watoto wao elimu, hivyo amewahimiza vijana kuacha kazi zisizo rasmi na kuchangamkia fursa zinazotolewa na kampuni hiyo.Naye Johnson Samirah kutoka Mkoa wa Njombe amesema uwepo wa kampuni ya ABT umekuwa mkombozi kwake huku akieleza kuwa kabla ya kuajiriwa alikuwa akiishi maisha magumu, lakini sasa ana uwezo wa kujitegemea na kutimiza ndoto zake.Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa kampuni, Frank Wales, msimamizi wa migodi inayomilikiwa na ABT, amesema lengo kuu la kampuni hiyo ni kuzalisha ajira nyingi kwa vijana ili kusaidia juhudi za Serikali katika kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini.Wales amebainisha kuwa kampuni imekuwa ikizalisha ajira nyingi kila mwaka kutokana na uwepo wa migodi mingi katika maeneo tofauti, ambapo kila mgodi unahusisha idadi kubwa ya vijana.“Kwa mwaka tumekuwa tukizalisha ajira nyingi, na kwa mwaka 2026 tumejipanga kuongeza uzalishaji zaidi, hivyo vijana wengi zaidi watahitajika,” amesema Wales.Ameongeza kuwa katika shughuli za uchimbaji, kampuni huzalisha mawe ya aina mbalimbali yakiwemo mawe ya mwamba na yenye madini.Hata hivyo ameongeza kuwa changamoto kubwa inayoikabili kampuni ni uhaba wa mitambo ya kisasa ya kuchakata mawe moja kwa moja, hali inayosababisha uzalishaji kuwa chini ya uwezo halisi.Kutokana na hali hiyo, kampuni ya ABT imetoa wito kwa wawekezaji kujitokeza kushirikiana nao, ikizingatiwa kuwa wana leseni nyingi za uchimbaji ambazo zinaweza kuongeza uzalishaji endapo zitatumika kikamilifu.“Tuna leseni nyingi, lakini hatuwezi kufanya kila kitu peke yetu tunakaribisha wawekezaji ili tushirikiane kuongeza uzalishaji na kutoa ajira zaidi,” amesisitiza Wales.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post