Wakati kanda ya Afrika Mashariki ikishuhudia ushindani mkali wa kutafuta umaarufu kupitia influencers (washawishi) wa mitandaoni, Tanzania imesisitiza kuwa mafanikio yake katika sekta ya utalii yanatokana na uhalisia na rasilimali zake zisizohitaji 'kupambwa mno' na gharama za serikali.
Kumekuwa na mjadala baada ya ziara ya YouTuber maarufu IShowSpeed nchi jirani, kuwa ziara hiyo ilikuwa ya kulazimisha ili kupandisha sifa za utalii wa majirani.
Pamoja na kelele zao za mtandaoni takwimu za Tanzania zinaonesha kutomhitaji IshowSpeed katika kutangaza utalii wake.
"Hatuogopi mbinu za kutafuta umaarufu, kwani ukweli wa mazingira yetu, kutoka Zanzibar hadi Serengeti, hauwezi kununuliwa kwa helikopta ya kukodi," alimalizia mchambuzi mmoja wa masuala ya utalii.
Hata hivyo, Rais Samia Suluhu Hassan, katika hotuba yake ya Sherry Party, ametoa jibu la kishindo kupitia takwimu.
"Tanzania haihitaji kutengeneza hadithi za kufikirika," alisema Rais Samia huku akionyesha kuwa mapato ya utalii yamefikia Dola bilioni 4 mwaka 2025. Huku majirani wakihaha kutafuta umaarufu kupitia TikTok na YouTube, Tanzania imejikita katika kuboresha miundombinu kama SGR na viwanja vya ndege ili kumfanya mtalii wa kawaida awe balozi wa nchi.
Kilimanjaro ni Moja, na Ipo Tanzania
Ni kama akijibu hoja za baadhi ya nchi jirani kujaribu kujimilikisha alama za Tanzania kama Mlima Kilimanjaro na utamaduni wa Kimaasai, Rais amesisitiza kuwa Dira ya 2050 italinda rasilimali hizo kama mali ya taifa. "Tunajiuza kwa kile tulichonacho. Utulivu wetu na asili yetu ndiyo sumaku kubwa zaidi duniani," aliongeza.
Mkakati wa 'Royal Tour' Unadunda
Wakati ziara za mastaa wa mtandaoni kama IShowSpeed zikiwa na maisha mafupi (viral for a day), mkakati wa Tanzania kupitia The Royal Tour unaendelea kuleta watalii wa kudumu na wawekezaji wakubwa.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment