Na Gift Mongi
Moshi
Baadhi ya shule za msingi kongwe katika kata ya Mwika Kusini katika jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro zimeanza kukarabatiwa ikiwa ni michango kutoka kwa wadau wa maendeleo sambamba na wananchi.
Shule hizo zinazoonekana kujengwa miaka mingi iliyopita hivyo kuwa na changamoto mbali mbali kama kuwepo kwa nyufa,kuchakaa kwa sakafu,mabati kutoboka na hata kutokuwa na pasta katika kuta kwenye baadhi ya majengo.
John Tarimo ni diwani wa kata hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya zoezi hilo alisema kubwa wananchi hao kwa ridhaa yao wamehamua kukarabati shule hizo badala ya kusubiri serikali iwafanyie kila kitu
"Wananchi wamehamasika na wakahamua sasa ni vyema kukarabati shule ili watoto wawe na mazingira mazuri zaidi ya kujifunzia ila ni mwendelezo wao katika kuunga mkono jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali"alisema Tarimo
Aidha alisema kuwa suala la maendeleo huletwa na wananchi wenyewe na hivyo kwa kuendelea kukarabati shule hizo kunaonesha ni jinsi gani wananchi hao walivyo na mwitikio mzuri wa watoto wao kupata elimu katika mazingira bora.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mawanda Evarist Shirima alisema kubwa jamii kwa sasa ina mwamko katika elimu na katika kudhihirisha hilo ndio maana jamii haijaachia kila kitu kwa serikali
Alisema shule yake ambayo ina jumla ya wanafunzi 75 imeanza kukarabatiwa na kuwa huo ni mwanzo mzuri katika kurudisha hadhi ya shule hiyo na hivyo wadau hao wa maendeleo hawana budi kuendeleza wema wao huo
"Tunaomba wadau wengine waendelee kujitokeza kwani huu ni mwanzo tu na hakika tutaenda kufika mbali maana imefurahishwa kuona jamii ina mwamko na sio kusubiri serikali hata kwa jambo ambalo lipo chini ya uwezo wetu"alisema
Mwisho

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254














Post a Comment