" ACHA BIA NA CHAPATI, PATA BIMA YA AFYA – RC CHALAMILA AWASHAURI WATANZANIA

ACHA BIA NA CHAPATI, PATA BIMA YA AFYA – RC CHALAMILA AWASHAURI WATANZANIA

Na Mwandishi wetu, Misalaba Media

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka Watanzania kubadili baadhi ya tabia za kila siku ili kujijengea uwezo wa kupata bima ya afya, akisema mabadiliko madogo ya matumizi yanaweza kuwa suluhisho kubwa kwa afya na uchumi wa familia.

‎Akizungumza mbele ya wananchi katika tukio la IST Festival lililofanyika Coco Beach Jijini Dar es Salaam, Chalamila amesema kwamba pesa zinazotumika kwenye starehe zisizo za lazima zinaweza kuelekezwa kwenye huduma muhimu za afya.

‎“Ukiacha kunywa bia kwa mwezi mmoja, una uwezekano wa kukata bima ya afya. Kama bia ni changamoto, hata kuacha chapati kwa muda kunaweza kusaidia kujenga afya bora kwa vizazi vyetu,” amesema Chalamila.

‎Aidha, Chalamila amempongeza Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuhimiza utekelezaji wa mpango wa kitaifa wa bima ya afya unaolenga kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za matibabu bila kuguswa na gharama.

‎Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwamba mpango wa bima ya afya ni hatua muhimu ya serikali katika kuimarisha ustawi wa jamii, kwani unarahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu katika hospitali mbalimbali nchini, bila kujali hali ya kifedha ya mgonjwa wakati wa dharura.

‎Chalamila amesisitiza kuwa maradhi hayachagui muda wala hali ya mtu, hivyo wananchi wanapaswa kujiandaa mapema kwa kujiunga na mifumo ya bima badala ya kusubiri kuugua ndipo waanze kutafuta suluhisho.

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post