Madereva wa pikipiki za kusafirisha abiria maarufu kama boda boda Manispaa ya Shinyanga wamepewa elimu ya kuacha tabia ya kukimbilia abiria ili kuepuka ajali zisizo za lazima.Elimu hiyo imetolewa na Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila ambapo amewataka kuweka utaratibu mzuri wa kubeba abiria ili kujiweka salama wao wenyewe na watumiaji wengine wa barabara Sajenti Ndimila amewataka madereva hao kuacha kukimbilia abiria Kwa kuwahiana kwani kunahatarisha maisha badala yake waweke utaratibu mzuri wa kubeba abiria kwenye vituo vyao vya usafirishaji utakao waweka wao salama pamoja na watumiaji wengine wa barabara ikiwa ni pamoja na kuleta sifa njema katika kazi Yao.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment