" HESLB INAVYOSHIRIKIANA NA WADAU KUWAWEZESHA WANAFUNZI KUJITEGEMEA KIUCHUMI

HESLB INAVYOSHIRIKIANA NA WADAU KUWAWEZESHA WANAFUNZI KUJITEGEMEA KIUCHUMI

Na: Dk. Reubeni Lumbagala, Misalaba Media -TangaElimu ni haki muhimu ya binadamu. Elimu ni nyenzo muhimu ya kumsaidia binadamu kumudu maisha yake. Kwa kutambua hilo, ndiyo maana wazazi na walezi wanapambana sana kusomesha watoto na vijana wao ili kuwawezesha kupata elimu bora ya kuwasaidia katika maisha yao na kutimiza ndoto zao za kimaendeleo walizonazo. Kazi kubwa na nzuri zimefanyika nchini katika kuboresha sekta ya elimu katika ngazi zote za elimu kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu Ili watoto na vijana wa Kitanzania waweze kupata elimu bora ya kuwasaidia maishani mwao. Mitaala ya ujifunzaji imeboreshwa ili kuwajengea wanafunzi umahiri wa kujitegemea pindi wanapohitimu ngazi mbalimbali za masomo yao.Ikumbukwe kuwa mabadiliko haya mazuri ya mitaala yamekuja kipindi hiki ambacho wahitimu wengi wana changamoto ya kukosa stadi na ujuzi stahiki wa kuwawezesha kuajiriwa au kujiajiri katika sekta mbalimbali. Ndiyo maana wengi tunapongeza mabadiliko haya ya mitaala kwa ustawi mwema wa wahitimu. Katika elimu ya juu, serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inaratibu zoezi la utoaji mikopo kwa wanafunzi huku wanufaika wa mikopo hiyo wakiwajibika kuirejesha mikopo hiyo baada ya kuhitimu na kuwa na kipato katika sekta rasmi au isiyo rasmi. Kwa kutambua changamoto iliyopo kwa baadhi ya wahitimu kukosa ujuzi na stadi mbalimbali, HESLB inashirikiana na taasisi mbalimbali zikiwemo taasisi ya kifedha katika kuhakikisha wanawajengea uwezo wahitimu ili waweze kuajiriwa au kujiajiri ambapo kufanikiwa kwao kunaiwezesha HESLB kukusanya fedha kutoka kwa wahitimu hao lakini pia nchi kupata wataalamu kwa maendeleo.Mathalani, Februari 18, 2026, katika Ofisi za CRDB Makao Makuu Jijini Dar es Salaam, HESLB iliingia makubaliano ya kushirikiana na CRDB Bank Foundation na kampuni ya Basil Link ili kuwawezesha wanafunzi wa vyuo vikuu kupata ujuzi wa kidigitali, elimu ya ujasiriamali na elimu ya fedha. Kwa hakika makubaliano haya ni mwelekeo mzuri katika kuwaandaa wanafunzi wa vyuo vikuu kujitegemea kutokana na mafunzo muhimu watakayoyapata kupitia uwezeshaji utakaofanywa hasa katika kuwa na jicho la kuona fursa za kiuchumi zilizopo. Kupitia programu hiyo lijulikanalo kwa jina la "Imbeju - SmartElite," wanafunzi wa vyuo watapata mafunzo ya ujasiriamali ili kuweza kujiajiri wenyewe. Aidha, watapata pia elimu ya fedha ambayo ni muhimu sana katika ulimwengu huu wa sasa. Sanjari na hilo, wanafunzi watapata mikopo nafuu na ushauri elekezi wa namna bora ya kuwekeza mikopo hiyo ili ilete tija kiuchumi. Katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Foundation, Tully Mwambapa alisema "Tunataka kuona vijana wanachangamkia fursa, wanabuni, wanaanzisha biashara na hata kuajiri wengine. Hii si tu kuwasaidia kumaliza chuo, bali kuwaandaa kuingia katika uchumi wa kidigitali wakiwa tayari na ujuzi pamoja na raslimali."Kwa upande wa Dk. Peter Mmari ambaye ni Mkurugenzi na Upangaji Mikopo wa HESLB amesema "Kupitia mpango huu, wanafunzi wataongeza uwezo wa kutumia mifumo ya kidijitali na watapata fursa ya kujiajiri wakiwa vyuoni au baada ya kuhitimu. Tunaamini wataweza pia kutoa mchango katika kuwainua Watanzania wengine kielimu na kiuchumi."Kimsingi, vijana wenye vipaji na mawazo bunifu watanufaika na mpango huu huku wakiwezeshwa mitaji na vitendea kazi kama kompyuta. Kwa hakika programu ya Imbeju - Smart Elite, ni mkombozi kwa vijana hasa katika ulimwengu wa uchumi wa kidijitali na biashara.


 

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post