Na mwandishi wetu Misalaba Media
Mbeya
Wakristo wametakiwa kuishi na kujenga imani yao mbele za Mungu.
Rai hiyo imetolewa na Mwinjilisti Doto Mwakalinga wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Samaria Shewa, linaloongozwa na Mchungaji Goodluck Mwakalinga.
Akinukuu maandiko kutoka Biblia katika Waebrania 11:1-8 na Isaya 58:14, Mwinjilisti Doto Mwakalinga amesema waumini wanapaswa kubeba na kudumisha imani, hivyo wanapaswa kumwangalia Mungu kama ilivyokuwa kwa Elisha baada ya Waisraeli kumuasi Mungu.
Aidha, akirejea kitabu cha 1 Wafalme 19:21, Mathayo 4:1 na Luka 5:27-28, amesema wanafunzi walipoacha kuvua samaki na kuamua kumtumikia Mungu walionesha utii mbele za Mungu.
Ameongeza kuwa nasi tunapaswa kuonesha utii ili tupate thawabu mbele za Mungu.
Mwinjilisti Mwakalinga amesema waumini wanapaswa kujifunza kwa Ibrahimu ambaye alikuwa tayari kumtoa mwanawe Isaka, kama ilivyoandikwa katika Mwanzo 22:17-18.
Amesisitiza kuwa tunapaswa kutii wito wa Mungu bila kujali nafasi tulizonazo.
Aidha, amesema waumini wengi wamekosa utii mbele za Mungu kwa kushindwa kumshukuru Mungu kupitia sadaka na mali zao.
Pia amewahimiza waumini kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato na kutoa sadaka ili Mungu awakumbuke.
Ameeleza kuwa ni vema kung’ang’ania katika maombi mbele za Mungu kama inavyoelekezwa katika Mhubiri 11:6, 2 Wafalme 2:9-10, Hesabu 1:16-17, Warumi 8:13-17, Wagalatia 5:12 na Matendo 2:39.
Akihitimisha, Mwinjilisti Doto Mwakalinga amesema Roho Mtakatifu ndiye kiongozi katika utumishi na katika Kanisa, hivyo waumini wanapaswa kujitahidi kuongozwa naye, kujitenga na uovu na kuyaacha matendo ya mwilini, kwa kuwa Roho Mtakatifu hukaa mahali palipo safi.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment