Na mwandishi wetu, Misalaba Media MbeyaHospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kushirikiana na Hospitali ya Aga Khan Tanzania zimesaini makubaliano ya ushirikiano (MoU) yenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Godlove Mbwanji, amesema kuwa lengo kuu la ushirikiano huo ni kubadilishana uzoefu, kuimarisha uwezo wa kitaalamu na kushirikiana katika utoaji wa huduma mbalimbali za afya kwa wananchi.“Lengo kubwa la kikao cha leo ni kusaini makubaliano yatakayowezesha taasisi hizi mbili kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya kuhudumia wagonjwa wetu,” amesema Dkt. Mbwanji.Dkt. Mbwanji ameongeza kuwa ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi una mchango mkubwa katika kuboresha huduma za afya nchini, huku ukichangia pia kukuza sekta ya tiba utalii kwa kuwavutia wageni kutoka nje ya nchi kuja kupata huduma bora za matibabu nchini Tanzania.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Aga Khan Tanzania, Dkt. Sisawo Konteh, amepongeza kusainiwa kwa makubaliano hayo akisema yatawanufaisha pande zote mbili kupitia ushirikiano wa karibu wa kimkakati katika utoaji wa huduma za afya na kujengeana uwezo wa kitaalamu.“Tunajivunia uwepo wa makubaliano haya kwani yatakuwa na manufaa kwa pande zote mbili, hususan katika kubadilishana uzoefu, kujengeana uwezo na kuendeleza ubunifu wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa taasisi zote mbili,” amesema Dkt. Konteh.Awali akizungumza na waandishi wa habari, Dkt. Mbwanji aliwahimiza wananchi kuendelea kujiunga na Bima ya Afya kwa Wote ili kujikinga na gharama kubwa za matibabu zinazoweza kujitokeza wanapokumbwa na changamoto za kiafya.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment