" HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YATOA ELIMU YA BIMA YA AFYA KWA WOTE KWA KUNDI LA WENYE WALEMAVU

HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YATOA ELIMU YA BIMA YA AFYA KWA WOTE KWA KUNDI LA WENYE WALEMAVU

Na Mwandishi wetu, Misalaba media MbeyaHospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kushirikiana na NHIF mkoa wa Mbeya wamekutana na kundi la watu wenye  ulemavu mkoa wa Mbeya kwa lengo la kutoa elimu ya umuhimu wa kujiunga na Bima ya Afya kwa wote.Akifungua kikao hicho leo tarehe 25 Februari 2026, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Godlove Mbwanji amesema lengo la kukutana na kundi hilo ni kuhakikisha wanapatiwa elimu ya umuhimu wa kujiunga na Bima ya Afya kwa eote, ikiwa ni miongoni mwa makundi maalumu yaliyopewa kipaumbele na Serikali ya Awamu ya Sita katika utekelezaji wa sheria hiyo" alisema Mbwanji."Serikali ya awamu ya Sita imepitisha sheria ya Bima ya Afya kwa kuanza na makundi maalumu ikiwemo wenye  walemavu na baada ya hapo itaendelea kwa watu wote hivyo tukaona tupate angalau uwakilishi ili nyinyi mnaoshiriki mafunzo haya muwe mabalozi na hivyo taratibu nyingine za kupata bima ziendelee.”  Dkt. MbwanjiKwa upande wake, msimamizi wa ofisi ya NHIF mkoa wa Mbeya, Bw. Nicolaus Mwangomo amesema miongoni mwa mada zilizotolewa ni pamoja na utaratibu wa uchangiaji, dhana ya Bima ya Afya kwa Wote pamoja na faida za kujiunga na huduma hiyo.Amesema utekelezaji huo ni sehemu ya ahadi ya Samia Suluhu Hassan ya kutekeleza sheria ya Bima ya Afya kwa wote."Nimekuwepo hapa kwa ajili ya kutoa elimu ya Bima ya Afya kwa wote kwa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu mkoa wa Mbeya kwa kuwapatia faida, utaratibu wa uchangiaji na dhana nzima ya bima hiyo "alisema  MwangomoAkizungumza kwa niaba ya washiriki, Bi. Rebecca Ramadhani ameshukuru kwa elimu waliyoipata, akieleza kuwa itasaidia kwa kiasi kikubwa watu wenye ulemavu kukabiliana na changamoto za matibabu wanazokutana nazo mara kwa mara."Nipende kushukuru kwa sababu mimi binafsi nimejifunza mengi kupitia semina hii na imetufundisha mengi hasa sisi watu wenye ulemavu tunaopitia changamoto nyingi, kwani itakuwa msaada mkubwa hasa katika eneo la matibabu"  Rebecca Ramadhani.Kikao hicho ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kuwa na bima ya afya, hasa kwa makundi maalumu, ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya kwa usawa na kwa gharama nafuu.


 

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post