Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Ziwa imetoa elimu kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kuhusu utekelezaji na usimamizi wa Sheria ya Bima nchini, hususan katika maeneo ya uchakataji wa madai ya wahanga wa ajali za barabarani. Elimu hiyo imelenga kuwajengea uwezo askari wa polisi ili kuhakikisha haki za wahanga zinalindwa kwa kuzingatia taratibu na matakwa ya kisheria.Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Afisa Ubora wa TIRA, Bw. Halfan Isango, amesema Jeshi la Polisi ni mdau muhimu katika utekelezaji wa Sheria ya Bima. Ameeleza kuwa taarifa na vielelezo vinavyokusanywa na Polisi wakati wa ajali vina mchango katika kurahisisha na kuharakisha uchakataji wa madai kwa waathirika."Ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi, kampuni za bima na TIRA utaondoa changamoto zinazojitokeza katika mchakato wa fidia kwa utekelezaji sahihi wa Sheria ya Bima utasaidia kuongeza uelewa wa wananchi, kuimarisha uwajibikaji, na kupunguza migogoro inayohusiana na madai ya ajali," alisisitiza Bw. Isango.Kwa upande wao, askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita wamepongeza TIRA kwa kutoa elimu hiyo, wakieleza kuwa imewasaidia kufahamu wajibu wao kisheria katika kulinda maslahi ya wahanga wa ajali za barabarani.Sambamba na mafunzo hayo, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini Kanda ya Ziwa inaendelea na zoezi la ukaguzi wa watoa huduma za bima na hali ya bima kwa vyombo vya moto mkoani Geita.


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment