" WAMILIKI WA BANDARI KAVU WASHAURIWA KUTOA HUDUMA KWA SAA 24 KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MIZIGO

WAMILIKI WA BANDARI KAVU WASHAURIWA KUTOA HUDUMA KWA SAA 24 KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MIZIGO

Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
‎Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Juma Mwenda, amewashauri wamiliki wa bandari kavu kuweka mazingira ya utoaji huduma kwa saa 24 ili kusaidia kupunguza malimbikizo ya mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam.‎Akizungumza leo Tarehe 19 Frebuari 2026 jijini Dar es Salaam katika mkutano wake na Kitengo cha Uendeshaji cha ICDs, Kamishna Yusuph Juma Mwenda amesema TRA inatambua kuwa bidhaa zote zinazoingia nchini hupitia katika bandari kavu, hivyo kuna umuhimu wa ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha ufanisi katika utendaji kazi.‎“Tumeona tukutane na nyie kwa sababu tunatambua kuwa Idara ya Forodha ya TRA haiwezi kufanya kazi bila nyie kutimiza wajibu wenu. Hivyo hakikisheni mnashirikiana nasi kulinda usalama wa Mtanzania,” amesema Mwenda.‎Aidha, amesema kutokana na ongezeko la mizigo kati ya mwaka jana na mwaka huu, ni muhimu kuweka mazingira wezeshi ya miundombinu pamoja na kuhakikisha huduma zinatolewa kwa saa 24, hususan nyakati za usiku, ili kuendana na kasi ya ukuaji wa biashara.‎Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Bandari Kavu (CIDAT), Meleckzedeck Shange, amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto za kimfumo, hasa wakati wa ukaguzi na uskanishaji wa mizigo, na kuomba maboresho yafanyike ili kuongeza ufanisi.‎“Kuna changamoto ndogo ndogo ambazo tunaamini zinaweza kuboreshwa na kufanya kazi iwe nyepesi zaidi kwa wote,” amesema Shange.‎Ameongeza kuwa kwa sasa matumizi ya bandari kavu yako katika takriban asilimia 62, lakini yanaelekea kufikia asilimia 90 kutokana na ongezeko kubwa la mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam. Amesema iwapo maboresho yatafanyika kwa wakati, kufikia mwaka 2026/2027 matumizi yanaweza kufikia kiwango hicho cha asilimia 90.

  

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post