Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Self Daud, ameuomba uongozi wa Mkoa wa Ruvuma kuzingatia pendekezo la kugawa wilaya hiyo ili kuunda halmashauri mbili zitakazosaidia kusogeza huduma karibu zaidi kwa wananchi. Amesema hatua hiyo itarahisisha utendaji kazi kwa watumishi wa umma na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za kijamiiAkizungumza katika kikao cha Baraza la Ushauri la Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa Songea Club uliopo ndani ya Manispaa ya Songea, Daud ameeleza kuwa ukubwa wa eneo la kiutawala la Tunduru pamoja na mtawanyiko wa kijiografia umekuwa changamoto katika kusimamia maendeleo kwa ufanisi. Ameongeza kuwa ongezeko la idadi ya watu, wingi wa kata na vijiji vinahitaji mpangilio mpya wa kiutawala ili kuimarisha usimamizi na uwajibikaji, hivo mgawanyiko huo utasaidia kuboresha ugawaji wa rasilimali za fedha na miundombinu, hatua itakayochochea maendeleo endelevu kwa wananchi🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment