" MAPINDUZI MAKUBWA YA KUWEZESHA WACHIMBAJI WADOGO

MAPINDUZI MAKUBWA YA KUWEZESHA WACHIMBAJI WADOGO


Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaKatika hatua ya kihistoria ya mageuzi ya Sekta ya Madini, Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imesaini makubaliano maalum na Benki ya CRDB yatakayorahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wachimbaji wadogo nchini.Makubaliano ya  hayo ya kihistoria yamesainiwa leo baina ya  CRDB  na Tume ya Madini Wakiingia saini; Songwe Gold Family Kupata Mkopo wa Sh50 Bilioni katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es salaam Februari 23, 2026 akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha mazingira ya uwekezaji na uwezeshaji katika sekta ya madini.Amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua za makusudi kujenga mazingira rafiki kwa wachimbaji wadogo kwa kuimarisha uchimbaji, biashara, kuongeza ufanisi na kukuza mchango wa sekta hiyo katika Pato la Taifa (GDP).“Tunawapongeza CRDB kwa kwenda ‘field’ kujionea uhalisia wa shughuli za uchimbaji na kufanya maamuzi kwa taarifa sahihi hili litaongeza tija ya uwekezaji, maendeleo ya sekta na mapato ya taifa,” amesema Mavunde.Waziri huyo amebainisha  kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zinazowatambua wachimbaji wadogo kisheria, huku Serikali ikiendelea kutoa leseni, na kufuta leseni za utafiti zisizoendelezwa na kugawa maeneo kwa wachimbaji wadogo ili kuongeza uzalishaji na tija.Songwe Gold Family Kuvunja Rekodi kwa Mkopo wa Sh50 Bilioni ni hatua iliyoelezwa kuwa ya kihistoria, Kikundi cha wachimbaji wadogo cha Songwe Gold Family kitakuwa cha kwanza nchini kupata mkopo wa Shilingi bilioni 50 kwa mkupuo kutoka CRDB — tukio ambalo halijawahi kutokea kwa wachimbaji wadogo.Aidha, Waziri Mavunde amesema Serikali iko katika hatua za mwisho za kuanzisha Mfuko wa Dhamana kwa ajili ya kukopesha wachimbaji wadogo ili kupunguza vikwazo vya upatikanaji wa mitaji na kuongeza kasi ya urasimishaji wa shughuli za uchimbaji.Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela amesemaCRDB: Mfumo Bunifu na Dhamana RafikiKwa wa  hivyo mpango huo ni wa kihistoria kwa benki na Sekta ya Madini kwa kuwa unaweka mfumo wa kisasa na shirikishi unaoendana na uhalisia wa wachimbaji wadogoKwa mujibu wa Nsekela, tayari benki hiyo imetoa Sh bilioni 186 kwa Sekta ya Madini; kati ya hizo, bilioni 136 kwa wachimbaji wakubwa na bilioni 50 kwa wachimbaji wadogo.Alieleza kuwa tofauti ya mpango huo ni aina ya dhamana, ambapo si lazima kutumia mali zisizohamishika pekee, bali dhamana zitajumuisha leseni halali za uchimbaji, leseni za biashara ya dhahabu, hifadhi ya dhahabu ya mkopaji pamoja na mikataba maalum.Serikali na Sekta Binafsi Kushirikiana ZaidiAkizungumza kwa niaba ya wachimbaji wadogo, rais wa FEMATA, John Bina, alisema mpango huo ulikuwa kilio cha muda mrefu cha wachimbaji wadogo na sasa unafungua ukurasa mpya wa maendeleo kwa sekta hiyo kwani   changamoto kuu kwa wachimbaji ni ukosefu wa mitaji, teknolojia na ushauri wa kitaalamu,  Kwa makubaliano hayo, wachimbaji wadogo wanatarajiwa kunufaika na mitaji, elimu ya kifedha na urasimishaji wa shughuli zao — hatua inayotarajiwa kuongeza uzalishaji, ajira na mchango wa Sekta ya Madini katika uchumi wa Taifa.

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post