" Mashabiki 18 wa Senegal wapata adhabu yao baada ya kufanya Vurugu AFCON

Mashabiki 18 wa Senegal wapata adhabu yao baada ya kufanya Vurugu AFCON

 

Mahakama Kuu ya Morocco imetoa hukumu kwa mashabiki 18 wa Senegal kufuatia matukio ya vurugu yaliyoripotiwa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo:

• Mashabiki tisa wamehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kila mmoja na kutozwa faini ya dola 500 za Marekani (Sh 1.3 milioni)

• Mashabiki sita wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kila mmoja pamoja na faini ya dola 200 (Sh 525,000).

• Mashabiki watatu wamehukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela kila mmoja na kutozwa faini ya dola 120 (Sh 312,000).

Hatua hiyo inaonyesha msimamo thabiti wa mamlaka za Morocco katika kukabiliana na vitendo vya vurugu na kuhakikisha nidhamu na usalama vinaimarishwa wakati wa matukio ya michezo.

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post