" Majibu ya Bodi kuhusu Dabi ya Kariakoo kati ya Simba SC na Yanga SC

Majibu ya Bodi kuhusu Dabi ya Kariakoo kati ya Simba SC na Yanga SC

 

Uongozi wa Simba SC umeiandikia barua Bodi ya Ligi (TPLB) kutaka kujua kwanini taarifa ya kuhamisha uwanja kutoka Benjamin Mkapa kwenda Amaan Complex ilitolewa kwanza na Afisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe badala ya Bodi ya Ligi TPLB na Bodi ikaja kutangaza siku yake ya pili ya Februari 16, 2026 baada ya Ali Kamwe kutangazwa jana yake Februari 15, 2026. Katika barua hiyo pia Simba Sports Club imehoji kanuni ipi imetumika kuhamisha uwanja maana ilitakiwa taarifa ya kuhamishwa kwa uwanja itoke kabla ya siku 21 kama kanuni inavyosema, taarifa ya kuhamishwa uwanja ilipaswa kutoka siku 21 kabla ya siku ya mechi husika

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeijibu Simba SC kufuatia malalamiko yao kuhusu uhamishaji wa mchezo wa Kariakoo Derby.

Kwa mujibu wa barua hiyo, Young Africans SC (Yanga) ndio wenyeji wa mchezo husika, na walipewa taarifa na wamiliki wa Uwanja wa Benjamin Mkapa kuwa siku ya derby kutakuwa na matumizi mengine ya uwanja huo.

Kutokana na hali hiyo, Yanga waliiomba TPLB kuruhusu mchezo uchezwe katika Uwanja wa New Amaan Complex. Bodi ya Ligi imeeleza kuwa ombi hilo lilikubaliwa kwa kuwa uwanja huo ulikuwa tayari umekaguliwa na kupitishwa na Kamati ya Leseni za Klabu ya TFF.

Aidha, TPLB imesisitiza kuwa Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, hana kosa lolote kwa kutoa taarifa hiyo, kwani mchakato wa maamuzi ulikuwa umeidhinishwa rasmi na mamlaka husika.

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post