
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mara imeandaa warsha maalum kwa lengo la kujadili matokeo ya uchambuzi wa mfumo wa utoaji huduma za afya katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda.Warsha hiyo pia imelenga kuweka mikakati madhubuti ya kuziba mianya ya rushwa iliyobainika ndani ya mfumo huo.Akizungumza katika warsha hiyo, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mara, Mohamed Shariff, alieleza kuwa moja ya majukumu makuu ya taasisi hiyo ni kuzuia vitendo vya rushwa nchini.Alibainisha kuwa uchambuzi uliofanywa katika mfumo wa utoaji huduma za afya Hospitali ya Bunda umeonesha uwepo wa mianya mbalimbali ambayo, kama ingeachwa bila kushughulikiwa, ingeweza kusababisha vitendo vya rushwa pamoja na upotevu wa mapato ya Serikali.Aidha, washiriki wa warsha hiyo walipokea na kujadili kwa kina matokeo ya uchambuzi huo, kwa lengo la kuweka maazimio yatakayowezesha utekelezaji wa mikakati ya kuzuia rushwa katika utoaji wa huduma za afya.Kwa upande wake, Dkt. Omari Ramadhan Mzee, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Rushwa kutoka TAKUKURU, alipongeza hatua hiyo na kuwataka washiriki kutimiza wajibu wao kwa uadilifu ili kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa.Pia aliwasilisha salamu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kutekeleza mikakati hiyo.Mgeni rasmi katika warsha hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Aswege Kaminyoge, alipongeza juhudi za TAKUKURU pamoja na Menejimenti ya Hospitali ya Bunda kwa hatua waliyochukua.Aliwataka wadau wote wa sekta ya afya kuzingatia maazimio yaliyowekwa, kwa kuyatekeleza kwa vitendo ili kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.Sambamba na hilo, aliagiza Ofisi ya Wilaya kuhakikisha inapata taarifa za utekelezaji wa maazimio hayo kwa ajili ya ufuatiliaji, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na endelevu kwa maslahi mapana ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.Warsha hiyo ilifanyika tarehe 19 Februari 2026, wilayani Bunda, katika ukumbi wa Balili Rock Resort, na iliwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya afya, wakuu wa idara, wahudumu wa afya pamoja na viongozi wa serikali na vyama.



🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment