" ‎MNEC KARIM NA MBUNGE BASHUNGWA WAUNGANA NA KAMATI YA SIASA YA MKOA KAGERA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KARAGWE

‎MNEC KARIM NA MBUNGE BASHUNGWA WAUNGANA NA KAMATI YA SIASA YA MKOA KAGERA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KARAGWE

 

Na Fabius Clavery, Misalaba Media-Kagera.

‎Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (MNEC) wa Chama Cha Mapinduzi, KarimAmri , ameungana na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa, pamoja na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Kagera kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

‎Katika ziara hiyo, viongozi hao wametembelea na kukagua jengo jipya la Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe ambalo linatarajiwa kukamilika muda wowote kuanzia sasa. Pia wamekagua jengo la kitega uchumi lililopo Omurushaka wilayani humo, likiwa ni sehemu ya miradi inayolenga kuongeza mapato na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

‎Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo, MNEC Karim amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fedha za maendeleo katika Jimbo la Karagwe, hatua iliyowezesha utekelezaji wa miradi hiyo pamoja na mingine ya kimkakati.

‎Amesema kukamilika kwa jengo la Halmashauri kutachochea ufanisi wa watumishi wa umma na kuboresha mazingira ya utoaji huduma kwa wananchi, huku akisisitiza umuhimu wa kusimamia ubora na thamani ya fedha katika miradi ya umma.

‎Kwa upande wake, Mbunge Innocent Bashungwa amesema Jimbo la Karagwe linaendelea kunufaika na uwekezaji wa Serikali katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu, afya, miundombinu na maji, akibainisha kuwa lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora karibu na maeneo yao.

‎Vilevile, viongozi hao wametembelea mradi wa vyumba vya kupangisha wa CCM katika Kata ya Buugene, mji mdogo wa Omurushaka. MNEC Karim amewataka wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili uanze kuzalisha mapato yatakayochangia shughuli za maendeleo.

‎Baadhi ya viongozi walioambatana na ziara hiyo wameeleza kuwa ukaguzi wa mara kwa mara wa miradi ni chachu ya kuhakikisha utekelezaji wake unakwenda sambamba na malengo yaliyokusudiwa.



  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment

Previous Post Next Post